Tulizonazo

Thursday, December 5, 2019

Mvua Afrika Mashariki: Vimbunga pacha kupiga Alhamisi, Ijumaa

Sambaza habari hii Facebook
Kimbunga
Vimbunga viwili vinatarajiwa kutua katika pwani ya Afrika Mashariki usiku wa leo Alhamisi na kesho Ijuamaa, mamlaka za hali ya hewa zinaripoti.
Eneo la Puntland nchini Somalia ndilo linalotarajiwa kuathirika zaidi na tufani hiyo.
Kwa mujibu wa wataalamu wa hali ya hewa, mgandamizo wa hali ya hewa ambao ulikuwa ukitengeneza vimbunga hivyo pacha umesababisha mvua kubwa katika nchi tisa za ukanda wa Afrika Mashariki.
Zaidi ya watu 130 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Kenya na Uganda

No comments:

Post a Comment