Na Deric Samora...
Bayern Munich hawatamfukuzia winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi
Bayern Munich hawatamfukuzia winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi katika kipindi cha dirisha la uhamisho mwezi Januari , lakini timu hiyo inaendelea kumumfuatilia Muingereza huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa lengo la kumnunua(Goal)
Mlinzi wa Bayern Munich David Alaba, ambaye mkataba wake katika klabu hiyo unamalizika msimu ujao, yuko makini kuhamia Real Madrid lakini timu hiyo ya uhispania inakabiliwa na ushindani kutoka Chelsea Paris St-Germain ambao wote wanataka kumsaini mchezaji huyo maarufu wa Austria mwenye umri wa miaka 28 (Marca)
Erling Braut Haaland anawindwa
Manchester City na Manchester United kwa pamoja wanatarajiwa kuelezea nia yao ya kumnunua mshambuliaji Mnorway ambaye kwa sasa anakipiga katika Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, katika miezi ijayo. (Mail)
Kiuongo wa kati wa Hungary na Red Bull Salzburg Dominik Szoboszlai, 20, yuko tayari kukataa wito wa kuhamia Arsenal na badala yake atajiunga na RB Leipzig katika kipindi cha uhamisho wa wachezaji mwezi Januari . (Sky Germany via Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Tottenham Harry Winks
Kiungo wa kati wa Tottenham Harry Winks, 24, yuko tayari kuzungumza na mwenyekiti wa klabu Daniel Levy kuhusu hofu yake juu ya hali yake ya baadaye na nafasi ta England katika msimu ujao wa kombe la Ulaya . (Telegraph - subscription required)
Meneja wa Leicester Brendan Rodgers amemwambia winga wa kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Demarai Gray kuwa asitarajie kujiunga na Foxes. (Mail)
Aston Villa washauriwa kutimiza matakwa ya Jack Grealish
Dean Smith anasema Aston Villa inapaswa kutimiza matakwa ya Jack Grealish ya kucheza Ulaya au au wakabiliwe na uwezekano wa kumpoteza kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 25. (Birmingham Mail)
Meneja wa Barcelona Ronald Koeman bado yuko makini katika kumsaini kiundo wa kati wa Mholanzi mwenye umri wa miaka 30 anayechezea Liverpool Georginio Wijnaldum. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Itakua vigumu kumuondoa Mshambuliaji wa Argentina katika klabu anayochezea
Kiungo wa kati wa Atletico Madrid Muhispania Koke, 28, amezungumzia jinsi anavyopenda kumshawishi mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33 kujiunga na Barcelona, lakini akakiri kuwa itakuwa vigumu "kwake kutoka huko ". (As)
Leicester na West Ham wanafuatilia taarifa kumuhusu kiungo wa kati wa Guinean Amadou Diawara, 23, ambaye inasemekana anaweza kuuwa na Roma. (Leicester Mercury)
Mshambuliaji wa Uruguayan Edinson Cavani, aliipenda Manchester united
Mshambuliaji wa Uruguayan Edinson Cavani, 33, alikataa kujiunga na Juventus na Inter Milan ili kujiunga na Manchester United kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao . (Sun)
Winga wa Leeds Raphinha, 23, anakiri kuwa alisikitishwa na uamuazi klabu ya ya Rennes wa kumuuza kwa klabu hiyo ya Primi Ligi bila Kufahamishwa. (ESPN Brazil via Goal)
Louis Saha anaamini Arsenal wanapaswa kumrejesha Olivier Giroud
Mshambuliaji wa zamani Louis Saha anaamini Arsenal inapaswa kuangalia uwezekano wa kumsaini tena Mfaransa Olivier Giroud mwenye umri wa miaka 34- kutoka Chelsea wakati wa msimu wa uhamisho wa wachezaji mwezi Januari (Metro)
hahara wa kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen huko Inter Milan huenda ukamfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kupunguzwa bei ya kurudi Ligi Kuu. (Telegraph - subscription required)
Kushindwa kusonga mbele kwa Red Bull Salzburg katika ligi ya mabingwa kumeongeza matumaini ya Arsenal kumsajili kiungo wa kati Dominik Szoboszlai mwezi Januari.(Football.London)
Hatahivyo, washika bunduki wanatarajia kukabiliana na upinzani kutoka kwa RB Leipzig, huku Bayern Munich na Real Madrid wakifikiriwa kuvutiwa naye. (Sky Sports)
No comments:
Post a Comment