Friday, January 5, 2024

Tetesi za sajili mbalimbali za soka barani ulaya ijumaa ya leo tarehe 05.01.2024

Na Deric Samora....

GFVB

Maelezo ya picha,

Roberto Firmino, 32, anataka kuondoka Al-Ahli ya Saudi Arabia

Fulham ni miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza ambavyo vimepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Liverpool, Roberto Firmino, 32, ambaye anataka kuondoka Al-Ahli ya Saudi Arabia . (Talksport)

Arsenal wamewasiliana na kiungo wa Everton na Ubelgiji, Amadou Onana, 22. (Teamtalk)

The Gunners pia wanajiandaa kumsajili mlinzi wa Uholanzi, Jorrel Hato mwenye umri wa miaka 17 kutoka Ajax . (Telegraph)

Borussia Dortmund itahitajika kutoa pauni milioni 25 ili kumnunua Muingereza, Jadon Sancho, 23, kutoka Manchester United. (Football Insider)

Atalanta inahitaji pauni milioni 51.7 kwa beki wao raia wa Italia, Giorgio Scalvini, 20, ambaye anahusishwa kwenda Manchester United. (Metro)

Kiungo wa kati wa Chelsea na England, Conor Gallagher, 23, anataka kusalia Stamford Bridge licha ya kuhusishwa na mpango wa kuondoka. (Mirror)

FGVB

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Thiago Silva huenda akarudi katika klabu yake ya zamani ya Fluminense

Mlinzi wa Chelsea raia wa Brazil, Thiago Silva, 39, atapewa nafasi ya kurejea katika klabu yake ya zamani ya Fluminense wakati wa majira ya joto. (Mirror)

Crystal Palace wanashughulikia mpango wa kumnunua beki wa Peterborough, Ronnie Edwards, 20. (Evening Standard)

Bournemouth wanatazamiwa kuwasilisha ombi la kumnunua kiungo wa Ecuador, Oscar Zambrano, 19, kutoka Quito . (Fabrizio Romano)

Beki wa pembeni wa Bayer Leverkusen, Mholanzi, Jeremie Frimpong, 23, anahusishwa na uhamisho, lakini klabu hiyo ya Ujerumani haina nia ya kumuuza. (Fabrizio Romano)

Middlesbrough wanakaribia kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland, Finn Azaz, 23, kwa pauni milioni 2 kutoka Aston Villa baada ya kiungo huyo kucheza kwa mkopo Plymouth Argyle. (Sky Sports)

Villa wanatarajiwa kuanza mazungumzo na winga wa Jamaica, Leon Bailey, 26, ambaye anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika klabu hiyo. (Mail)

Paris St-Germain wako mstari wa mbele kutaka kumsajili kipa wa England na Manchester United, Mary Earps, 30. (Evening Standard)

Bayern Munich wanamfuatilia beki wa AC Milan, Muingereza Fikayo Tomori, 26. (Sky Germany)

Endelea kufuatilia blog yetu kwa kila yanayojiri pia kwa habari mbalimbali tutafute kupitia whatsApp +255753864398

No comments:

Post a Comment