
Kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari , huku klabu ya Real Madrid ikiwa na matumaini ya kuanzisha mazungumzo ya kupunguza bei ya Man United ya £126.4m ili kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa huku akiingia miezi 12 ya mwisho katika kandarasi yake. (L'Equipe via AS)
Tottenham imeendeleza hamu yake ya kutaka kumnunua mchezaji wa Ajax Donny van de Beek , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 na raia wa Uholanzi anataka kuhamia Real Madrid, ambao wanajiandaa kutoa dau la £46.2m (De Telegraaf via FourFourTwo)
Manchester City na Chelsea wamekuwa na mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji wa Barcelona Ousmanne Dembele mwenye umri wa miaka 22 (Eldesmarque via Sun)
- ‘Je ni De Bruyne ama McTominay atakayeamua debi ya Manchester?'
- Ndani ya saa 24 ambazo ziliushangaza ulimwengu wa ndondi
- Messi atunukiwa tuzo ya mchezaji bora
Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard anaweza kupata zaidi ya £150m kutumia baada ya marufuku ya uhamisho ya klabu hiyo kupunguzwa huku ikiwalenga winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, pamoja na beki wa kushoto wa Leicester City na Uingereza Ben Chilwell, 22.. (Mail)

Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, ambaye amesalia na miezi 18 katika kandarasi yake amejiondoa katika mazungumzo ya kumuongezea kandarasi na yuko tayari kuondoka msimu ujao.. (Mirror)
No comments:
Post a Comment