Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aweka jiwe la msingi Ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 likipita juu ya Ziwa Victoria litakalounganisha Mkoa wa Mwanza na Geita.
Mradi huo pia utahusisha ujenzi wa barabara unganishi wenye urefu wa Kilomita 1.6 na fedha zote za utekelezaji zinatokana na mapato ya ndani.
Alipotangaza uamuzi wa kujenga daraja eneo hilo wakati wa ziara zake kadhaa mkoani Mwanza, Rais Magufuli alisema kukamilika kwa mradi huo siyo tu kutarahisisha usafiri na usafirishaji, bali pia utaondoa adha ya wagonjwa kupoteza maisha wakati wakisubiri vivuko vinavyotoa huduma eneo hilo.
Eneo la Kigongo – Busisi linahudumiwa na vivuko viwili vya Mv Mwanza ambacho ni kipya na Mv Misungwi ambazo hutumia wastani wa dakika 30 hadi 40 kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine.
Alichokisema Rais Magufuli katika uzinduzi wa daraha hilo
“Nawapongeza wana Mwanza na Watanzania kwa ujumla kwa kutekeleza mradi huu mkubwa wa kimaendeleo, pia nawapongeza wote walioshiriki kufanikisha ujenzi wa daraja hili”
“Kwangu mimi ujenzi wa daraja hili ni uthibitisho mwingine kwamba nchi yetu sio masikini na kwamba sisi kama Watanzania nia tunaweza”
“Nikiwa uwanja wa CCM Kirumba wakati naomba kura niliahidi kujenga daraja hili, lakini wapo waliosema haliwezekani, niliona hili tukiamua sisi kama watanzania tutaweza”
“Mradi huu unatekelezwa na serikali ya Tanzania, ni fedha za Watanzania, hizi ni kodi zenu, Tanzania sisi ni matajiri”
“Mkandarasi wa mradi huu hakikisha mnaukamilisha mapema ikiwezekana hata kabla ya muda, kwa sababu mradi huu ni muhimu kwa maendeleo ya watanzania, hizi ni fedha za Watanzania.
No comments:
Post a Comment