Tetesi za soka ulaya na Deric Samora
Paris St-Germain wanamtaka kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 28, lakini klabu hiyo ya Ufaransa itahitajika kuwauza baadhi ya wachezaji wake kwanza. (Sky Sports)
Arsenal inajiandaa kuwasilisha dau la pauni milioni 30 kumnunua kipa wa Sheffield United Muingereza Aaron Ramsdale, 23. (TalkSport)
Robert Lewandowski(kushoto) akisherehekea kufunga bao dhidi ya Chealsea Mei 2020
Chelsea imezengumza na ajenti wa mshambuliaji wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland Robert Lewandowski, 32, kuhusu uwezekano wa kumleta Stamford Bridge. (Bild, via Sun)
Gunners hata hivyo wametakiwa kuongeza ofa ya Ramsdale kwa zaidi ya pauni milioni 32 baada ya ofa zao mbili za awali kukataliwa. (Times)
Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham
Chelsea wako tayari kumuachilia mshambuliaji Tammy Abraham kujiunga na mahasimu wao wa Ligi ya Premia Arsenal kwa mkopo. Tottenham na West Ham pia wanamnyatia kungo huyo matata aliye na umri wa miaka 23. (Sun)
Mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner, 25, ameanzisha mazungumzo ya kuondoka Chelsea msimu huu wa joto. Kuna uwezekano akarejea katika ligi yake nyumbani Bundesliga. (90min)
No comments:
Post a Comment